Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza kutoka Mashhad, Sheikh Talal Abdulrahman, mpigania uhuru wa Palestina na msimamizi wa jalada la wafungwa wa Harakati ya Muqāwama wa Kiislamu ya Hamas, Jumatano usiku, katika webinari ya nne ya kimataifa iliyokuwa na anuani isemayo “Iran ya Kiislamu; Uwanja wa heshima ya Kiislamu katika kukabiliana na utawala wa Kizayuni”, iliyofanyika kwa njia ya mtandao, baada ya kuwakumbuka na kuwapa heshima mashahidi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Palestina, Lebanon, Yemen na Iraq, alisema: Suala la Palestina, tangia siku za mwanzo za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu, daima limekuwa ni suala la msingi na lisilokubaliwi kufanyiwa biashara ya kisiasa katika ajenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Alieleza kuwa: Iran haikuchukua msimamo wa kisiasa wa muda mfupi tu, bali mwendo wake umejengwa juu ya uongozi wa Kimungu na uelewa wa kina wa uadilifu wa Mwenyezi Mungu, akasema: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, katika kipindi cha miaka mingi, imelipa gharama kubwa kwa ajili ya kuwatetea waliodhulumiwa na kusimama dhidi ya utawala wa Kizayuni na Marekani—gharama zilizojumuisha vikwazo, mazingira ya kuzingirwa, vitisho na mauaji ya kulengwa—lakini kamwe haikurudi nyuma kutoka katika misingi na njia yake.
Msimamizi wa jalada la wafungwa wa Harakati ya Hamas, akirejea nafasi ya Marekani kama mhimili wa mradi mpya wa kikoloni katika eneo, alisisitiza: Katika wakati ambapo serikali nyingi zilijiondoa katika misimamo ya muqāwama, msimamo thabiti wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ulikuwa nembo ya heshima, utu na uhuru wa Umma wa Kiislamu. Leo, dalili za kudhoofika kwa haiba ya utawala wa Kizayuni na kushindwa kwa Marekani kulazimisha mapenzi yake zinaonekana waziwazi.
Sheikh Talal Abdulrahman alieleza kuwa uungaji mkono wa Iran kwa muqāwama wa Palestina na Lebanon umetolewa bila masharti yoyote ya kisiasa, na akaongeza: Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaiona muqāwama kuwa ni haki, wajibu na heshima; na operesheni ya Tufani ya Al-Aqsa ni mfano ulio wazi wa matunda ya uungaji mkono wa kimkakati na endelevu wa Iran kwa muqāwama wa Palestina.
Akiashiria kuundwa kwa mhimili wa kweli wa muqāwama wenye nyanja nyingi za mapambano katika eneo, alisema: Leo, mizani mpya ya kuzuia na kuhodhi nguvu imeundwa dhidi ya utawala wa Kizayuni, na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran bado inahesabiwa kuwa uti wa mgongo wa mhimili huu, ikiendelea kuhifadhi nafasi yake muhimu katika kuuthibitisha na kuukuza.
Mpigania uhuru huyu wa Palestina, kwa kutoa shukrani kwa uungaji mkono na misimamo ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, alisema: Damu ya mashahidi kamwe haitapotea bure; Tufani ya Al-Aqsa ni mwanzo wa njia ya muqāwama, si mwisho wake; na utawala wa Kizayuni, hata kama muda utapita, umehukumiwa kimaumbile kuelekea kwenye maangamizi.
Alitoa pia pongezi kwa juhudi za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuwaunga mkono wapigania uhuru na waliodhulumiwa katika eneo, na akaongeza: Uungaji mkono huu ni mfano unaotoa msukumo na funzo kwa Umma wa Kiislamu katika kukabiliana na dhulma na uvamizi.
Maoni yako